Victoria government logo
coronavirus.vic.gov.au

Ushauri wa kiafya na vizuizi (Health advice and restrictions) - Kiswahili (Swahili)

Ushauri wa kudhibiti na kujikinga dhidi ya COVID-19.

Ikiwa unahitaji mkalimani, pigia simu Huduma ya Kutafsiri na Ukalimani kwa 131 450.

Jilinde wewe mwenyewe na wengine dhidi ya COVID-19

COVID-19 bado inaenea katika jamii. Bado inaweza kuwafanya watu wengine kuwa wagonjwa sana. Kujilinda ni njia bora ya kuwalinda wengine. Huwezi kueneza COVID ikiwa hupati COVID.

Nenda ukapimwe

Kaa nyumbani na upime antijeni ya haraka (RAT) ikiwa:

 • una dalili kama vile mafua ya pua, koo ya kuumwa, kikohozi, homa, au baridi.
 • wewe ni mtu mwenye mawasiliano na mtu aliye na COVID-19.

Ikiwa kipimo chako ni hasi, unapaswa kuendelea kutumia vipimo vya haraka vya antijeni kwa siku chache zijazo na ukae nyumbani hadi dalili zako ziondoke.

Ikiwa kipimo chako ni chanya kwa kutumia kipimo cha haraka cha antijeni unapaswa kuripoti matokeo yako kwa Idara ya Afya. Unaweza kutoa taarifa ya matokeo kwenye mtandaoExternal Link au kwa kupiga simu 1800 675 398. Ukiripoti matokeo yako, unaweza kupata huduma ya matibabu na dawa za COVID bila malipo.

Uliza daktari akupime PCR ikiwa unakuwa mgonjwa sana na COVID-19. Hauhitaji kuripoti matokeo yako ikiwa ulipimwa chanya kuwa umeambukizwa kutoka kwenye kipimo cha PCR.

Tafuta habari zaidi kwenye Pata Kipimo cha COVID-19External Link .

Tunza afya yako

Iwapo utathibitishwa kuwa na COVID-19 katika kipimo unapaswa kupumzika na kuzungumza na daktari wa kawaida. Watu wengi watakuwa na dalili kidogo na wanaweza kupona wakiwa nyumbani. Unalazimika:

 • Kukaa nyumbani kwa angalau siku 5. Usiende kazini au shuleni. Kaa mbali na hospitali, vituo vya utunzaji wa wazee na huduma za walemavu.
 • Vaa barakoa ikiwa ni lazima kuondoka nyumbani kwa dharura. Barakoa bora ni zile za upasuaji au N95.
 • Waambie watu ambao umeonana nao au maeneo ambayo umetembelea hivi karinbuni kwamba una COVID.

Dalili zako zikizidi, unapaswa kuongea na GP au uwasiliane na Kliniki ya Kupumua ya GPExternal Link .

Unaweza pia kupiga simu Nambari ya Msaada ya Kitaifa ya Virusi vya KoronaExternal Link kwa 1800 020 080.

Pigia simu Idara ya Dharura ya Mtandaoni ya VictoriaExternal Link kwa huduma ya haraka ikiwa huwezi kuongea na GP.

Kwa dharura piga simu Sifuri Mara Tatu (000).

Unaweza kuambukiza wengine kwa hadi siku 10. Unapaswa kukaa nyumbani ikiwa una mafua pua, koo ya kuumwa, kikohozi, homa, baridi, kutokwa na jasho, au upungufu wa kupumua. Tumia kipimo cha antijeni cha haraka au zungumza na GP ikiwa huna uhakika.

Msaada

Kwa habari zaidi:

Kuzungumza na mtu:

Uliza kuhusu dawa za COVID

Dawa za COVID huokoa maisha na kuzuia watu kuugua sana COVID-19. Zinapaswa kuchukuliwa mapema iwezekanavyo na ndani ya siku 5 baada ya kuugua ili kufanya kazi vizuri zaidi.

Jibu maswali hayaExternal Link ili kujua kama unastahiki dawa za COVID. Zungumza na GP kama unaona kuwa unastahiki. Daktari anaweza kusaidia kuhakikisha watu wanaostahiki wanapata matibabu haraka

Kwa habari zaidi tazama Dawa za kuzuia virusi na dawa zingineExternal Link .

Vaa barakoa

Barakoa zinaweza kukuzuia kupata na kueneza COVID-19. Barakoa zinapaswa kuwa za ubora mzuri na zinazoenea uso vizuri. Barakoa za N95 na P2 (vipumuaji) zinatoa ulinzi zaidi.

Unapaswa kuvaa barakoa:

 • kwenye usafiri wa umma, ndani ya nafasi ya umma, na nje katika sehemu yenye watu wengi.
 • ikiwa una COVID-19 na unalazimika kuondoka nyumbani
 • ikiwa wewe au yupo na mtu aliye katika hatari kubwa ya kuugua sana.

Watoto wenye umri wa miaka 2 au chini lazima kuacha kuvaa barakoa kwani kuna hatari ya kubanwa na kukosa hewa.

Kwa habari zaidi tazama Barakoa za usoExternal Link .

Pata dozi yako inayofuata ya chanjo

Chanjo ni njia bora ya kujikinga wewe na familia dhidi ya kuugua sana COVID-19. Unapaswa kudungwa chanjo zilizopendekezwa kwako kwa wakati. Ongea na GP ili kujua ni dozi ngapi zinazopendekezwa.

Bado unapaswa kupata chanjo ikiwa umekuwa na COVID-19. Tumiakitafuta kliniki ya chanjoExternal Link ili uweke nafasi ya dozi yako inayofuata kwa GP au duka la dawa la karibu nawe.

Kwa habari zaidi tazama Chanjo ya COVID-19External Link .

Wezesha hewa safi iingie

COVID-19 inaenea hewani. Kuleta hewa safi ndani ya chumba kunaweza kupunguza hatari ya kueneza COVID-19. Fungua madirisha au milango inapowezekana unapokusanyika na wengine ndani ya nyumba. Ikiwa huwezi, unaweza kutumia kisafishaji hewa kinachobebeka (kichujio cha HEPA) ambacho huondoa chembe za erosoli kutoka hewani.

Kwa habari zaidi tazama Uingizaji hewaExternal Link .

Kupona kutokana na COVID-19

Watu wengi watajisikia vibaya kutokana na COVID-19 baada ya kutokuwa na maambukizi tena. Ruhusu mwili wako kupata wakati wa utunzaji na kupona vizuri.

Unapaswa kusubiri miezi 3 baada ya kuambukizwa, kabla ya kupata dozi yako inayofuata ya chanjo. Hii itahakikisha unapata ulinzi bora dhidi ya virusi.

Unaweza kupata COVID-19 tena kwa haraka kama wiki 4 baada ya kupata nafuu. Ikiwa una dalili wiki 4 au zaidi baada ya kuambukizwa, unapaswa kupimwa.

COVID ndefu ni wakati dalili za COVID-19 hudumu kwa zaidi ya miezi 3. Unapaswa kuonana na daktari wako ambaye anaweza kukusaidia kudhibiti dalili zako au kukuelekeza kwa mtaalamu ikiwa hii itahitajika.

Pata maelezo zaidi kuhusu COVID ndefuExternal Link .

Ikiwa wewe ni mtu wa mawasiliano

Uko katika hatari ya kuugua COVID-19 ikiwa unaishi nyumba moja au umekuwa mtu wa karibu na mtu ambaye amepimwa kuwa anaumwa.

Unapaswa kufuatilia dalili na upime mara kwa mara kwa siku 7 baada ya kuwasiliana na mtu ambaye amepimwa kuwa anaumwa. Katika kipindi hiki, inashauriwa:

 • epuka hospitali, vituo vya kulelea wazee, na huduma za walemavu
 • vaa barakoa unapotoka nyumbani, ikijumuisha kwenye usafiri wa umma na katika maeneo ya ndani kama vile kazini na shuleni
 • ruhusu hewa safi kwenye nafasi za ndani kwa kufungua madirisha, inapowezekana

Kwa habari zaidi kuhusu Orodha hakiki ya mawasilianoExternal Link .

Reviewed 08 December 2022

Coronavirus Hotline

Call the Coronavirus Hotline if you need help to report a rapid antigen test (RAT) or if you have any questions about COVID-19.

The Victorian Coronavirus Hotline diverts to the National Coronavirus Helpline every night between 4pm and 9am.

Please keep Triple Zero (000) for emergencies only.

Was this page helpful?