vic_logo
coronavirus.vic.gov.au

Safari na usafiri (Travel and transport) - Kiswahili (Swahili)

Jifunza zaidi juu ya mabadiliko kwa usafiri wa umma, karantini na safari za majimbo na ng'ambo.

Unaweza kupata habari zaidi katika Kiingereza kwenye kurasa yetu ya safari na usafiri.

Ikiwa unahitaji msaada zaidi katika lugha yako, unaweza kupiga simu TIS Taifa kwenye 131 450 na ombe kwa mkalimani, ndipo omba kuunganishwa na kituo cha simu ya Usafiri wa Umma wa Viktoria kwenye 1800 800 007.

Mpango wa Kupata Kibali cha Usafiri (Victorian Travel Permit Scheme)

Kuanzia saa 12 jioni (6pm) Jumatatu, 11 Januari 2021 utapaswa kuomba kibali cha kuingia Victoria kutoka kwa mahali popote Australia.

Mpango wa kibali ni kwa ajili ya wasafiri na wakaaji wa Victoria na ambao wanarudi nyumbani.

Victoria watatofuatisha mahali pengine Australia kama rangi ya kijani, rangi ya machungwa au rangi ya nyekundu ikitegemea hatari ya coronavirus katika eneo hilo.

Ili kuomba kibali, itakubidi kutoa maelezo kuhusu mahali unapotoka na mahali unapokwenda.

Watu wanaoishi katika jumuiya za mpakani hawatahitaji kibali lakini watapaswa kutoa uthibitisho kuhusu anwani yao mpakani.

Jinsi ya kuomba:

Omba kibali kwa kutembelea Service Victoria

Maeneo yahusu kibali

Eneo la rangi ya nyekundu ina maana kwamba huwezi kuingia Victoria. Lakini kuna sababu zingine zitakazokuruhusu kuingia, kwa mfano, kibali cha Specified Worker au Freight Workers, au cheti cha ruhusa kwa ajili ya huduma ya huruma. Ikiwa utaingia kutoka kwa eneo la rangi ya nyekundu bila vyeti hivi au cheti cha kazi, utapewa faini na kugeuzwa.

Eneo la rangi ya machungwa ina maana kwamba utaweza kuomba kibali na itakupasa kupata kipimo kabla ya masaa 72 kupita tangu ulipoingia Victoria. Lazima ukae nyumbani kabla na baada ya kipimo chako, mpaka umepokea matokeo ya hakuna virusi.

Eneo la rangi ya kijani ina maana kwamba utaweza kuomba kibali na kuingia Victoria. Baada ya kuingia Victoria unapaswa kuangalia kwa dalili na kupimwa ikiwa unajisikia mgonjwa.

Vibali vya kuruhusiwa kwa sababu maalum

Unaweza kuomba kibali cha kuruhusiwa kwa sababu maalum ikiwa kuna sababu maalum. Kama hizi:

  • wakati wa maisha kukaribia kwisha au mazishi
  • unarudi kwa sababu ya ugonjwa, afya, kutunza mtu au kutoa huduma ya huruma
  • lazima uingie kwa sababu ya dharura
  • kutunza mnyama ambaye yuko upande wa pili ya mpaka.

Reviewed 15 January 2021

24/7 Coronavirus Hotline

If you suspect you may have coronavirus (COVID-19) call the dedicated hotline – open 24 hours, 7 days.

Please keep Triple Zero (000) for emergencies only.

Was this page helpful?